Jinsi ya Kubadilisha TahasusiJinsi ya Kubadilisha Tahasusi

Jinsi ya Kubadilisha Tahasusi (Combination) TAMISEMI 2026, Kubadilisha Tahasusi TAMISEMI 2026, Mfumo wa SELFORM TAMISEMI, Jinsi ya kubadili combination Kidato cha Tano, Tahasusi za Kidato cha Tano 2026.

Baada ya matokeo ya uchaguzi wa Kidato cha Tano (Form Five Selection) kutoka, changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wengi ni kupangiwa tahasusi (combination) ambayo hawakuwa wameiweka kipaumbele au ambayo hawaipendi.

Habari njema ni kuwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hutoa fursa ya kufanya mabadiliko hayo kupitia mfumo wa kielektroniki wa SELFORM. Huu hapa ni mwongozo wa hatua kwa hatua wa namna ya kubadilisha tahasusi yako mwaka 2026.

Vigezo vya Kuzingatia Kabla ya Kubadilisha Tahasusi

Kabla ya kuanza mchakato huu, ni lazima ujiridhishe na mambo yafuatayo:

  1. Ufaulu wa Masomo (D au Zaidi): Lazima uwe na ufaulu usiopungua alama ‘D’ katika masomo yote matatu yanayounda tahasusi unayotaka kuhamia.

  2. Pointi za Tahasusi (Cut-off Points): Kila tahasusi ina kiwango chake cha chini cha ufaulu (pointi). Mfumo hautakuruhusu kuhamia tahasusi ambayo pointi zako za ufaulu hazifikii kigezo.

  3. Nafasi Katika Shule: Mabadiliko yanategemea uwepo wa nafasi katika shule uliyopangiwa au shule unayotaka kuhamia.

Hatua kwa Hatua za Kubadilisha Tahasusi Mtandaoni

Hatua ya 1: Ingia Kwenye Mfumo wa SELFORM

Tembelea tovuti ya TAMISEMI na ufungue mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi kupitia link hii: selform.tamisemi.go.tz.

Hatua ya 2: Fungua Akaunti Yako (Login)

Ingia kwa kutumia namba yako ya mtihani wa Kidato cha Nne (Index Number) na neno la siri (password) ulilotumia wakati wa kujaza fomu za uchaguzi wa shule shuleni kwenu.

Hatua ya 3: Fungua Sehemu ya Maombi ya Mabadiliko

Baada ya kuingia, tafuta sehemu iliyoandikwa “Request Change” au “Maombi ya Mabadiliko”. Hapa utaona maelezo ya tahasusi uliyopangiwa kwa sasa.

Hatua ya 4: Chagua Tahasusi Mpya

Chagua tahasusi unayohitaji kulingana na machaguo yatakayotolewa na mfumo. Mfumo wa SELFORM umesetiwa kuonyesha tahasusi ambazo sifa zako za ufaulu zinaruhusu tu.

Hatua ya 5: Thibitisha na Tuma (Submit)

Baada ya kufanya uchaguzi wako, bonyeza kitufe cha “Save” au “Confirm Changes”. Utapokea ujumbe wa uthibitisho kuwa maombi yako yamepokelewa na yanafanyiwa kazi.

Nini cha Kufanya Ikiwa Dirisha la Mtandaoni Limefungwa?

Ikiwa dirisha la SELFORM limefungwa na tayari umeripoti shuleni, unaweza kufanya mchakato huu kwa njia ya barua:

  • Andika barua ya maombi kwenda kwa Mkuu wa Shule uliyopangiwa.

  • Ambatanisha matokeo yako ya NECTA na eleza sababu za kutaka kubadili tahasusi.

  • Mkuu wa shule atapitia maombi yako na akijiridhisha kuwa una sifa na nafasi ipo, atakuhamishia kwenye tahasusi husika na kutoa taarifa TAMISEMI.

Mchakato wa kubadilisha tahasusi unahitaji umakini mkubwa. Hakikisha unachagua masomo unayoyamudu ili uweze kufanya vizuri katika mtihani wako wa Kidato cha Sita.

Endelea kutembelea matokeoyanectatz.com kwa taarifa za haraka kuhusu kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho na mabadiliko ya masomo.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *