Fomu Za Kujiunga Na Form One 2025/2026 Kidato cha Kwanza (Download PDF)
Baada ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza (Form One Selection 2026) kutangazwa na TAMISEMI, hatua muhimu inayofuata kwa sasa ni kupata Fomu za Kujiunga (Joining Instructions).
Wazazi na walezi wengi wamekuwa wakiuliza, “Je, ninaipataje fomu ya shule aliyopangiwa mwanangu?”
Katika ukurasa huu wa matokeoyanectatz.com, tumekuwekea utaratibu rahisi wa kupakua fomu hizo kwa shule zote za Serikali ili uweze kuandaa mahitaji ya mwanafunzi mapema kabla ya tarehe ya kufungua shule.
Fomu za Kujiunga ni Nini?
Fomu za Kujiunga (au Joining Instructions) ni waraka rasmi unaotolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari. Waraka huu unaelezea:
-
Sare za Shule: Rangi ya shati, sketi/suruali, na aina ya viatu.
-
Mahitaji ya Bweni/Kutwa: Vifaa anavyopaswa kwenda navyo mwanafunzi (mfano: godoro, ndoo, vyombo).
-
Sheria za Shule: Taratibu ambazo mwanafunzi anapaswa kuzifuata.
-
Tarehe ya Kuripoti: Siku rasmi ya kufika shuleni.
Jinsi ya Kupakua Fomu za Form One 2025 (Mtandaoni)
Mwaka huu, Serikali imerahisisha zoezi hili. Huna haja ya kusafiri hadi shuleni kufuata fomu. Unaweza kuipakua kupitia simu yako kwa kufuata hatua hizi:
-
Tembelea Mfumo wa TAMISEMI: Bofya link ya selection.tamisemi.go.tz.
-
Tafuta Jina la Mwanafunzi: Nenda kwenye Mkoa -> Wilaya -> Shule ya Msingi aliyotoka.
-
Angalia Upande wa Kulia: Mbele ya jina la mwanafunzi na shule aliyopangiwa, kuna kitufe au maandishi yameandikwa “Joining Instruction”.
-
Pakua (Download): Bofya hapo na fomu itafunguka kama PDF. Ihifadhi kwenye simu yako na uende kuiprinti (Chapisha).
Pakua Fomu Hapa (Orodha ya Mikoa)
Ili kukurahisishia, tumekuorozeshea link za mikoa yote hapa chini. Ukibonyeza mkoa wako, utaona orodha ya shule na fomu zake:
| Mikoa (A – G) | Mikoa (I – M) | Mikoa (N – Z) |
| Arusha | Iringa | Njombe |
| Dar es Salaam | Kagera | Pwani |
| Dodoma | Katavi | Rukwa |
| Geita | Kigoma | Ruvuma |
| Kilimanjaro | Shinyanga | |
| Lindi | Simiyu | |
| Manyara | Singida | |
| Mara | Songwe | |
| Mbeya | Tabora | |
| Morogoro | Tanga | |
| Mtwara | Zanzibar | |
| Mwanza |
Mambo ya Kuzingatia Kwenye Fomu
Unapopata fomu hiyo, kuwa makini na mambo yafuatayo ili usipate usumbufu siku ya kuripoti:
-
Mishono ya Sare: Baadhi ya shule zina mishono maalum. Usishone sare kwa fundi yeyote kabla ya kuona maelekezo au picha kwenye fomu.
-
Namba ya Usajili (Admission Number): Baadhi ya fomu zina namba ya usajili wa mwanafunzi, ihifadhi vizuri.
-
Malipo Benki: Kama kuna michango ya lazima (iliyoidhinishwa), fomu itaonyesha Akaunti Namba ya Benki ya Shule. USITUME PESA KWA NAMBA YA SIMU YA MTU BINAFSI.
Unahitaji Msaada?
Kama umejaribu kupakua fomu na inagoma, au huioni fomu ya shule yako, inawezekana Mkuu wa Shule bado hajaliweka kwenye mfumo (Upload).
Katika hali hiyo:
-
Subiri kidogo na jaribu tena baadae.
-
Nenda shule ya msingi aliyosoma mwanao, walimu wakuu mara nyingi hupewa nakala za fomu hizo.
-
Tuandikie hapa chini kwenye Comment jina la shule unayoitafuta.
MatokeoYaNectaTZ.com inawatakia maandalizi mema ya kuanza Kidato cha Kwanza 2026.
Tafadhali SHARE ukurasa huu na wazazi wengine ili nao wapate fomu zao kirahisi.
