Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRAMajina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili TRA – Machi 2026,Usaili TRA 2026, Kuitwa kwenye usaili TRA, Sekretarieti ya Ajira, Ajira Portal, Nafasi za kazi TRA.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anawataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali kuwa usaili unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 09 Machi 2026 hadi 16 Machi 2026.

Wasailiwa wanapaswa kuzingatia tarehe, muda, na mahali pa usaili kama ilivyoainishwa kwa kila kada.

Ratiba na Maeneo ya Usaili

Usaili huu utahusisha hatua mbalimbali kulingana na kada husika:

  • Usaili wa Mchujo (Aptitude Test): Utafanyika katika maeneo tofauti yaliyoainishwa kwenye tangazo.

  • Usaili wa Mahojiano (Oral Interview): Utafanyika kufuatia ratiba ya kila kada.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

Ili kuruhusiwa kufanya usaili, hakikisha unazingatia vigezo hivi vya lazima:

  • Vyeti Halisi (Original Certificates): Fika na vyeti halisi kuanzia Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, na Shahada. Result slips na Testimonials hazitakubaliwa kabisa.

  • Kitambulisho: Lazima uwe na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi (NIDA, Mpiga Kura, Pasipoti, n.k.).

  • Namba ya Usaili: Kila msailiwa anapaswa kuingia kwenye akaunti yake ya Ajira Portal na kunakili namba yake ya usaili.

  • Barakoa (Mask): Ni lazima kuvaa barakoa (mask) unapofika eneo la usaili.

  • Gharama: Msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi.

     

Pakua Orodha Kamili ya Majina ya Usaili TRA (PDF)

Bonyeza link hapa chini kuona majina yote ya walioitwa, tarehe, na kumbi za usaili:

LINK YA PDF HAPA

Zingatia: Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana kwenye tangazo hili, tafadhali ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal kuona sababu za kutokuitwa kwako.

Kila la heri kwa wasailiwa wote wa TRA!

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *