Nafasi ya Kazi TPSC: Assistant Lecturer Project Management (Februari 2026), Ajira TPSC 2026, Nafasi za kazi Chuo cha Utumishi wa Umma, Project Management Jobs Tanzania, Ajira mpya za wahadhiri 2026, Ajira Portal TPSC.
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimetangaza nafasi mpya ya ajira kwa upande wa kitaaluma. Nafasi hii ni kwa ajili ya Assistant Lecturer (Project Management) kwa mwezi Februari 2026. Kama wewe ni mtaalamu wa usimamizi wa miradi au uchumi, hii ni fursa yako ya kujiunga na utumishi wa umma.
Nafasi hii inahitaji mtu mwenye weledi wa hali ya juu katika kufundisha, kufanya tafiti, na kutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala ya miradi.
Muhtasari wa Nafasi ya Kazi
-
Mwajiri: Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)
-
Nafasi: Assistant Lecturer (Project Management)
-
Idadi ya Nafasi: 1
-
Mshahara: Ngazi ya PHTS 2/1
-
Mwisho wa Maombi: 22 Februari 2026
Majukumu ya Kazi (Job Responsibilities)
Mteule katika nafasi hii ya mhadhiri msaidizi atakuwa na majukumu yafuatayo:
-
Kufundisha: Kutoa mafunzo na kufanya tathmini (exams/tests) kwa wanafunzi wa ngazi ya Shahada ya Kwanza (NTA Level 8).
-
Maandalizi ya Masomo: Kuandaa miongozo ya kufundishia na vifaa vya mazoezi ya darasani.
-
Tafiti na Semina: Kufanya tafiti za kitaalamu, kuongoza semina, na kuchambua mifano ya miradi (case studies).
-
Usimamizi: Kusimamia na kusahihisha miradi ya mwisho ya wanafunzi (Final Year Projects).
-
Kazi Nyingine: Kutekeleza majukumu yote atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Sifa na Vigezo Vinavyohitajiwa
Ili maombi yako yazingatiwe, ni lazima uwe na sifa zifuatazo:
-
Elimu: Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) katika fani ya Project Management au Economics kutoka chuo kinachotambulika na serikali.
-
Ufaulu wa Kiwango cha Juu:
-
Shahada ya Kwanza (Bachelor): GPA kuanzia 3.5 na kuendelea.
-
Shahada ya Uzamili (Masters): GPA kuanzia 3.8 na kuendelea.
-
Namna ya Kutuma Maombi (How to Apply)
Maombi yote yanapokelewa kidijitali kupitia mfumo wa ajira wa serikali. Hakikisha unatuma maombi yako kabla ya saa tano na dakika 59 usiku wa tarehe 22 Februari 2026.
Hatua za kufuata:
-
Tembelea tovuti ya Recruitment Portal ya serikali.
-
Ingia (Login) au jisajili kama huna akaunti.
-
Tafuta nafasi ya Assistant Lecturer – TPSC (Project Management).
-
Ambatanisha nyaraka zako (CV, Vyeti vya Kidato cha nne, sita, na Vyuo).
Zingatia: Hakikisha vyeti vyako vimeunganishwa vizuri kwenye mfumo ili kuepuka maombi yako kukataliwa.
