TAMISEMI Yatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza

TAMISEMI Yatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026 (Form One Selection)

Hatimaye penye nia pana njia. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) leo imetangaza rasmi orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026.

Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema jumla ya wanafunzi 937,581 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za Serikali nchi nzima.

Hii ni habari njema kwa wazazi na wanafunzi waliokuwa wakisubiri kwa hamu majina haya tangu matokeo ya Darasa la Saba yatangazwe.

Mchanganuo wa Takwimu za Selection 2026

Katika tangazo hilo, Prof. Shemdoe amebainisha takwimu muhimu za uchaguzi wa mwaka huu kama ifuatavyo:

  • Jumla ya Waliochaguliwa: Wanafunzi 937,581.

  • Wasichana: 508,477.

  • Wavulana: 429,104.

  • Wenye Mahitaji Maalum: Wanafunzi 3,228 (Wasichana 1,544 na Wavulana 1,684).

  • Idadi ya Shule: Wanafunzi hawa wamepangwa katika shule za sekondari za Serikali 5,230.

Wanafunzi hawa ni wale waliopata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 katika Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi 2025.

Tarehe Rasmi za Kufungua Shule (Reporting Dates)

Waziri amesisitiza kuwa muhula wa masomo utaanza rasmi mwezi Januari. Tarehe za kuripoti zimegawanywa kama ifuatavyo:

  1. Wanafunzi wa Bweni (Boarding): Wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 12 Januari, 2026.

  2. Wanafunzi wa Kutwa (Day): Wanatakiwa kuripoti na kuanza masomo tarehe 13 Januari, 2026.

“Nawaagiza Ma RC, Ma RAS, Ma DC, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Shule kuhakikisha wanakamilisha maandalizi yote ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza,” alisisitiza Prof. Shemdoe.

Aina za Shule Walizopangiwa

Prof. Shemdoe ameleeza kuwa wanafunzi wamepangwa katika makundi mbalimbali kulingana na ufaulu na nafasi:

  • Shule za Bweni (Special Schools): Kwa wenye ufaulu wa juu zaidi.

  • Shule za Ufundi (Amali).

  • Shule za Bweni za Kitaifa.

  • Shule za Kutwa (Ward Schools): Ambazo ni nyingi zaidi.

Maagizo Mazito ya Serikali

Ili kuhakikisha azma ya Elimu Msingi Bila Malipo inatimia, Serikali imetoa maagizo yafuatayo:

  1. Kwa Viongozi (RCs, DCs, DEDs): Kuhakikisha hakuna vikwazo vyovyote kwa wanafunzi kuanza masomo na kuhakikisha miundombinu imekamilika.

  2. Kwa Wazazi na Walezi: Kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, wanahudhuria, na kubakia shuleni hadi watakapohitimu.

  3. Kwa Wanafunzi: Kuitumia vizuri fursa hii kwa kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na matarajio ya wazazi.

Jinsi ya Kuangalia Majina na Joining Instructions

Orodha kamili ya majina ya wanafunzi na Fomu za Maelezo ya Kujiunga (Joining Instructions) kwa shule za bweni zinapatikana sasa.

Bofya Link Hapa Chini Kuona Majina:

BOFYA HAPA KUONA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2026

Pia unaweza kupakua fomu za kujiunga (Joining Instructions) kupitia tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).

Chanzo cha Taarifa: James K. Mwanamyoto Dar es Salaam Taarifa imetolewa na Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI).

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *