RASMI NECTA Kutangaza Tarehe ya Matokeo ya Kidato cha NneRASMI NECTA Kutangaza Tarehe ya Matokeo ya Kidato cha Nne

RASMI NECTA Kutangaza Tarehe ya Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeweka wazi kuwa litafanya mkutano muhimu na waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE) 2025 siku ya tarehe 31 Januari, 2026. Huu ni wakati ambao maelfu ya wanafunzi nchini kote wamekuwa wakiusubiri kwa hamu kubwa ili kufahamu hatma ya masomo yao ya sekondari.

Katika picha rasmi iliyotolewa na Baraza, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, ndiye atakayeongoza mkutano huo kutoa mwelekeo wa ufaulu kwa mwaka huu.

Maelezo ya Mkutano wa NECTA Januari 31

Kulingana na taarifa hiyo, haya hapa ni mambo muhimu unayopaswa kuzingatia:

  • Tarehe ya Mkutano: Jumamosi, tarehe 31 Januari, 2026.

  • Muda: Saa 5:00 Asubuhi.

  • Eneo: Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dar es Salaam.

  • Mubashara (Live): Mkutano huu utarushwa kupitia YouTube Necta online.

Maandalizi ya Kupokea Matokeo ya CSEE 2025

Huku tukiwa tunaelekea tarehe hiyo ya kihistoria, matokeoyanectatz.com inakushauri kuanza kujiandaa mapema kwa kutunza namba yako ya mtihani. Mara tu Prof. Said A. Mohamed atakapohitimisha mkutano wake, matokeo yatawekwa rasmi kwenye tovuti.

Jinsi ya Kuwa wa Kwanza Kupata Matokeo:

  1. Hifadhi (Bookmark) tovuti yetu ya matokeoyanectatz.com.

  2. Hakikisha una bando la kutosha kuanzia asubuhi ya tarehe 31.

  3. Fuatilia YouTube Necta online ili kusikia takwimu za jumla za ufaulu kabla ya kuangalia namba yako.

Bonyeza hapa kwenda kwenye ukurasa wa matokeo ya form four necta results 2025/2026

Siku ya mwangaza imekaribia! Tarehe 31 Januari 2026 saa tano asubuhi ndiyo itakuwa mwisho wa subira. Tunawatakia kila la kheri wanafunzi wote waliofanya mitihani ya Kidato cha Nne mwaka 2025.

Je, una hofu au shauku yoyote kuelekea tarehe 31 Januari? Tuandikie kwenye maoni hapa chini, na endelea kubaki nasi kwa updates za kila saa!

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *