Nafasi Za Kujitolea JKTNafasi Za Kujitolea JKT

Nafasi Za Kujitolea JKT 2026 PDF FILE, JKT Kujitolea 2026: Nafasi, Sifa na Ratiba ya Usaili Mikoani (Tangazo Rasmi)

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa Wito wa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2026. Tangazo hili lililotolewa leo tarehe 20 Januari, 2026, na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, linawahusu vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani wenye nia ya kulitumikia taifa lao.

Kupitia tovuti ya matokeoyanectatz.com, tumekuchambulia kila kitu unachopaswa kujua ili uweze kufanya maombi yako kwa usahihi na kwa wakati.

Maombi na Utaratibu wa Kuchaguliwa

Utaratibu wa vijana kuomba nafasi hizi haufanyiki mtandaoni moja kwa moja, bali unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya mahali ambapo mwombaji anaishi. Hivyo, vijana wanatakiwa kufuatilia maelekezo ya ziada kutoka kwa wakuu wao wa maeneo husika.

Sifa za Kipaumbele: Taaluma za IT na Michezo

Katika awamu hii ya JKT Kujitolea 2026, jeshi limeweka kipaumbele kwa vijana wenye taaluma za teknolojia na vipaji vya michezo. Vijana wenye sifa zifuatazo wanahimizwa kujitokeza kwa wingi:

Vipaji vya Michezo: Vijana wenye uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali.

Ngazi ya Diploma: ICT, Computer Science, Information Technology, Business Information Systems, na Cyber Security.

Ngazi ya Degree (Bachelor): Computer Engineering, IT, Computer Science, Business IT, na Cyber Security and Digital Forensics.

Ratiba ya Usaili na Kuripoti Makambini

Ni muhimu kuzingatia tarehe hizi ili usipoteze sifa za kuteuliwa:

Tarehe ya kuanza Usaili: Usaili utaanza rasmi tarehe 26 Januari 2026 katika mikoa yote nchini.

Kipindi cha Kuripoti: Kwa wale watakaoteuliwa, wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT kuanzia tarehe 27 Februari 2026 hadi 04 Machi 2026.

Malengo ya Mafunzo ya JKT

Jeshi la Kujenga Taifa limesisitiza kuwa mafunzo haya yanalenga kuwajengea vijana:

Uzalendo na Umoja wa Kitaifa.

Ukakamavu na Stadi za Maisha.

Stadi za Kazi ili kuwasaidia vijana kujiajiri wenyewe baada ya kumaliza mkataba wao.

Zingatia: JKT imeweka wazi kuwa halitoi ajira wala halihusiki kuwatafutia vijana ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama au mashirika ya serikali.

JKT PDF FILE

Vifaa na Maelekezo ya Ziada

Kwa maelezo zaidi kuhusu sifa za jumla na vifaa unavyotakiwa kwenda navyo makambini, tembelea tovuti rasmi ya JKT ya www.jkt.mil.tz.

Endelea kufuatilia matokeoyanectatz.com kwa habari za uhakika kuhusu nafasi za kazi, matokeo ya necta, na fursa mbalimbali za kimasomo nchini Tanzania.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *