Assistant Lecturer Economic and FinanceAssistant Lecturer Economic and Finance

Nafasi ya Kazi IAA Arusha: Assistant Lecturer Economic and Finance (Februari 2026), Ajira IAA 2026, Assistant Lecturer Jobs Tanzania, Nafasi za kazi Economics and Finance, Ajira Portal Tanzania 2026, Ajira mpya IAA Arusha.

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimetangaza nafasi ya kazi ya Assistant Lecturer (Economic and Finance). Nafasi hii ni fursa murua kwa wenye Shahada ya Uzamili (Masters) wanaotaka kufanya kazi katika mazingira ya kitaaluma na kutoa mchango wao katika sekta ya uchumi na fedha nchini Tanzania.

Kama unazo sifa za ufundishaji na ufaulu wa hali ya juu, chukua hatua sasa na uombe nafasi hii kabla ya tarehe ya mwisho.

Muhtasari wa Nafasi ya Kazi

  • Mwajiri: Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

  • Nafasi: Assistant Lecturer (Economic and Finance)

  • Idadi ya Nafasi: 1

  • Mshahara: Ngazi ya PHTS 2

  • Mwisho wa Kutuma Maombi: 22 Februari 2026

Majukumu ya Kazi (Job Responsibilities)

Mteule katika nafasi hii ya Mhadhiri Msaidizi atakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kufundisha: Kutoa mihadhara (Lecturing) kwa wanafunzi hadi ngazi ya Shahada ya Kwanza (NTA Level 8).

  2. Maandalizi ya Masomo: Kuandaa nyenzo za kujifunzia na miongozo ya kufundishia (Teaching Manuals).

  3. Tafiti na Semina: Kufanya tafiti za kisayansi, kuongoza semina, na kuchambua mifano ya matukio (Case Studies).

  4. Usimamizi: Kusimamia miradi ya wanafunzi (Student Projects) na tafiti zao za mwisho.

  5. Ushauri wa Kitaalamu: Kutoa huduma za ushauri na huduma kwa jamii chini ya usimamizi.

Sifa na Vigezo Vinavyohitajiwa

Ili uweze kufikiriwa katika nafasi hii, lazima uwe na sifa zifuatazo za kitaaluma:

  • Elimu: Shahada ya Uzamili (Master’s Degree) katika fani ya Economics and Finance au fani inayolingana nayo kutoka chuo kinachotambulika.

  • Ufaulu (GPA):

    • Shahada ya Kwanza (Undergraduate): GPA isiyopungua 3.5.

    • Shahada ya Uzamili (Postgraduate): GPA isiyopungua 3.8.

  • Ujuzi wa Ziada: Uwezo wa kufanya tafiti na kuandaa machapisho ya kitaaluma.

Namna ya Kutuma Maombi (How to Apply)

Maombi yote yanapokelewa kupitia mfumo rasmi wa ajira wa serikali (Ajira Portal). Hakikisha unapakia nyaraka zako zote muhimu (CV na Vyeti) kwa usahihi.

Hatua za kufuata:

  1. Ingia kwenye tovuti ya portal.ajira.go.tz.

  2. Tafuta nafasi ya Assistant Lecturer Economic and Finance.

  3. Bonyeza ‘Apply’ na kamilisha hatua zote.

  4. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 Februari 2026.

>>Tuma maombi hapa

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *