Jinsi ya Kubadili Combination Form Five 2026/2027 TAMISEMI
Je, umepangiwa combination ambayo huipendi au unaona utashindwa kuisoma? Usiwe na wasiwasi. Wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano 2026/2027 wanatafuta jinsi ya kubadili combination TAMISEMI ili kusoma michepuo wanayoipenda kama PCM, PCB, HGL, HKL, au EGM.
Katika makala hii, matokeoyanectatz.com tutakupa hatua kwa hatua za kufuata ili kubadili mchepuo wako kisheria na kwa urahisi.
Je, Inawezekana Kubadili Combination Baada ya Kupangiwa?
Jibu ni NDIYO. TAMISEMI inaruhusu wanafunzi kubadili combinations, lakini mchakato huu haufanyiki kiholela. Kuna vigezo na taratibu maalum zinazopaswa kufuatwa ili mabadiliko hayo yakubalike kwenye mfumo wa serikali.
Vigezo vya Kubadili Combination 2026
Kabla ya kuanza mchakato, hakikisha unakidhi vigezo hivi:
-
Ufaulu (Cut-off Points): Lazima uwe na ufaulu unaostahili (angalau Alama ‘C’ tatu) kwenye masomo ya combination unayotaka kwenda.
-
Nafasi Katika Shule: Shule uliyopangiwa lazima iwe na nafasi kwenye mchepuo unaouhitaji.
-
Idhini ya Mkuu wa Shule: Mkuu wa shule uliyopangiwa ndiye msimamizi mkuu wa mchakato huu katika ngazi ya shule.
Hatua za Kubadili Combination Form Five (Step-by-Step)
1. Ripoti Shuleni Kwanza
Wanafunzi wengi hukosea kwa kutokwenda shule waliyopangiwa. Kanuni ya kwanza ni kuripoti kwenye shule uliyopangiwa na TAMISEMI na kukamilisha usajili wa awali.
2. Andika Barua ya Maombi
Andika barua rasmi ya kuomba kubadili mchepuo kwenda kwa Mkuu wa Shule. Kwenye barua hiyo, taja:
-
Mchepuo uliochaguliwa na TAMISEMI.
-
Mchepuo unaotaka kusoma.
-
Sababu za msingi (Mfano: Una ufaulu mzuri zaidi kwenye masomo ya mchepuo mpya au unalenga fani fulani chuoni).
3. Uhakiki wa Sifa
Mkuu wa shule atahakiki cheti chako cha matokeo ya Kidato cha Nne (NECTA Result Slip) ili kuona kama una sifa za kusoma mchepuo huo mpya.
4. Mabadiliko Kwenye Mfumo (Selform MIS)
Mabadiliko yakishakubaliwa shuleni, Mkuu wa shule kupitia kwa mwalimu wa taaluma atafanya mabadiliko hayo kwenye mfumo wa TAMISEMI Selform MIS. Hii ni muhimu ili utambulike rasmi na serikali kama mwanafunzi wa mchepuo huo.
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQs)
1. Je, naweza kubadili combination na shule kwa wakati mmoja? Hili ni gumu kidogo. Kubadili shule (Transfer) kunahitaji kibali kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) au TAMISEMI makao makuu, na mara nyingi hufanyika baada ya muhula wa kwanza kuanza.
2. Je, kuna malipo yoyote kubadili mchepuo? Hapana. Utaratibu wa kubadili combination ni bure. Epuka matapeli wanaoweza kudai pesa ili “wakusaidie.”
3. Nifanye nini nikikataliwa kubadili shuleni kwangu? Ikiwa shule haina nafasi au haina mchepuo unaoutaka, unaweza kuomba uhamisho wa kwenda shule nyingine yenye mchepuo huo kupitia taratibu za uhamisho wa wanafunzi (Student Transfer).
Kubadili combination ni haki yako ikiwa una sifa za kutosha. Hakikisha unafanya maamuzi haya mapema kabla masomo hayajachanganya.
Kumbuka: Endelea kufuatilia matokeoyanectatz.com kwa ajili ya updates za haraka kuhusu Selection na miongozo ya kujiunga na vyuo.
