Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha TanoWaliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano

Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2026/2027 (TAMISEMI Selection),form five selection 2026/2027

Je, unatafuta waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano 2026/2027? Baada ya matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE 2025) kutangazwa na NECTA, kiu ya kila mwanafunzi na mzazi ni kujua shule aliyopangiwa kuendelea na masomo ya juu ya sekondari.

Katika makala hii ya matokeoyanectatz.com, tutakuelekeza jinsi ya kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa (Selection za Form Five) kupitia mfumo wa TAMISEMI (Selform MIS), na tutatoa link ya PDF ya majina yote punde tu yatakapotangazwa rasmi.

Lini TAMISEMI Atatangaza Selection za Form Five 2026?

Kwa kawaida, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hutoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati kuanzia mwezi Mei au Juni.

Uchaguzi huu unategemea mambo makuu mawili:

  • Ufaulu wa mwanafunzi (Credit za masomo ya tahasusi/combination husika).

  • Nafasi za shule zilizopo nchi nzima.

Jinsi ya Kuangalia Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2026/2027

Ili kuona shule uliyopangiwa, unaweza kutumia njia mbili rahisi:

1. Kupitia Tovuti ya TAMISEMI (Online Portal)

  1. Tembelea tovuti rasmi ya selection: selection.tamisemi.go.tz au selform.tamisemi.go.tz.

  2. Chagua sehemu iliyoandikwa “Selection 2026”.

  3. Tafuta Mkoa wako, kisha Wilaya, na mwisho shule uliyosoma (O-Level).

  4. Orodha ya majina itatokea na shule walizopangiwa.

2. Kupitia PDF (Download Link)

Mara nyingi tovuti ya TAMISEMI hulemewa na “traffic” kubwa. Hapa matokeoyanectatz.com, tutaweka link ya moja kwa moja kudownload PDF ya majina yote kwa mikoa yote ya Tanzania (Bara).

PAKUA PDF HAPA: Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano

Mikoa Inayohusika na Selection 2026

Selection hizi zitahusisha wahitimu kutoka mikoa yote, ikiwemo:

  • Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma.

  • Mbeya, Iringa, Tanga, Kilimanjaro.

  • Kagera, Mara, Morogoro, Pwani, na mingineyo.

Nini cha Kufanya Ukikosa Jina Kwenye Selection?

Usikate tamaa! Ikiwa jina lako halipo kwenye awamu ya kwanza (First Selection), kuna uwezekano wa kutokea kwenye Awamu ya Pili (Second Selection). Pia, unaweza kuomba kujiunga na Vyuo vya Kati (VETA na NACTE) kupitia mfumo huo huo wa TAMISEMI.

Muhimu: Joining Instructions 2026

Baada ya kuona jina lako, hatua inayofuata ni kupata Joining Instructions (Maelekezo ya kujiunga na shule). Hii ni fomu inayoeleza mahitaji ya shule, sare, na tarehe ya kuripoti. Hakikisha unaipakua kwenye tovuti ya shule uliyopangiwa au mfumo wa TAMISEMI.

Endelea kutembelea matokeoyanectatz.com kwa habari za uhakika kuhusu Elimu Tanzania.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *