Matokeo ya Young Africans vs Al Ahly Leo (23/01/2026) – Hatua ya Makundi CAFCL
Na Mwandishi Wetu, Cairo Ijumaa, Januari 23, 2026
Mtanange wa kukata na shoka kati ya miamba ya soka barani Afrika, Al Ahly SC dhidi ya Young Africans SC (Yanga), unaochezeka usiku wa leo katika dimba la Al Salam mjini Cairo. Huu utakua mchezo wa mzunguko wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (Group B).
Hapa chini tutakuweke matokeo ya mchezo huo mara tu utakapo anza kuchezwa
Matokeo ya Mechi:
-
Al Ahly [ 0 ] – [ 0 ] Yanga SC
Historia Inasemaje? (H2H)
Rekodi za hivi karibuni zinaonesha kuwa Yanga wameanza kuwa “mfupa mgumu” kwa Al Ahly. Katika mara tano za mwisho walizokutana:
-
Machi 2024: Al Ahly 1-0 Yanga
-
Desemba 2023: Yanga 1-1 Al Ahly
-
Aprili 2016: Al Ahly 2-1 Yanga
Licha ya Al Ahly kuwa na rekodi bora nyumbani, Yanga wameonesha kukua kimataifa na safari hii wamedhamiria kuvunja mwiko wa kutopata ushindi nchini Misri.
Jinsi ya Kufuatilia (LIVE Updates)
Mchezo utaanza kurindima saa 1:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki (19:00 EAT). Mashabiki nchini Tanzania wanaweza kutazama mbashara kupitia Azam Sports 2 au kupitia viungo vya LIVE Streaming kwenye kurasa za kijamii za matokeoyanectatz.com.
Utabiri wa Mtaalamu:
“Mchezo utakuwa wa mbinu nyingi. Yanga watacheza kwa kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushtukiza kupitia kwa Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua. Al Ahly watamiliki mpira, lakini kama Yanga watakuwa makini kwenye ulinzi, sare nyingine au ushindi mwembamba wa ugenini unawezekana.”
Endelea kubaki nasi Matokeoyanectatz.com kwa matokeo ya papo hapo, kikosi rasmi (lineups) na uchambuzi wa baada ya mechi.
