TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA (JSC)TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA (JSC)

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA AWALI – TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA (JSC)

Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) inapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa tarehe 17 Novemba, 2025, kuwa orodha ya majina ya waliochaguliwa kufanya Usaili wa Awali (Initial Interview) imetoka.

Usaili huu utafanyika kwa Njia ya Kielektroniki katika vituo mbalimbali vilivyoainishwa kulingana na mikoa waliochagua waombaji.

RATIBA YA USAILI KWA KADA MBALIMBALI:

Usaili utafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Desemba, 2025 kama ifuatavyo:

  • Jumanne, 16 Desemba 2025: Afisa Utumishi II (Rasilimaliwatu) na Afisa Ununuzi II.

  • Jumatano, 17 Desemba 2025: Afisa Ugavi, Afisa Ugavi Msaidizi I, na Hakimu Mkazi II.

  • Alhamisi, 18 Desemba 2025: Mhasibu II na Msaidizi wa Ofisi.

  • Jumatatu, 22 Desemba 2025: Dereva II na Mlinzi.

  • Jumanne, 23 Desemba 2025: Kompyuta Operata II na Mpishi II.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

  1. Muda: Usaili utaanza saa 2:30 Asubuhi (au muda mahususi ulioainishwa kwenye jedwali la kila kada).

  2. Vyeo Halisi: Wasailiwa wote lazima wafike na vyeti vyao halisi vya Elimu, Taaluma, Cheti cha Kuzaliwa na Kitambulisho chenye picha kinachotambulika na Serikali.

  3. Kutohudhuria: Wasailiwa watakaofika bila nyaraka tajwa au kuchelewa hawatasailiwa.

  4. Matokeo: Watakaofaulu hatua hii ya kwanza ndio watakaotaarifiwa kwa ajili ya usaili wa ana kwa ana (Oral) au vitendo (Practical).

Tafadhali pakua faili la PDF hapa chini ili kuona jina lako, kituo chako cha kufanyia usaili, na tarehe husika.

 LINK YA PDF HAPA

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *