Kalenda ya Shule 2026, Public Holidays,Tarehe za Kufungua na Kufunga Shule
Mwaka wa masomo 2026 unapoanza, ni muhimu kwa wazazi, walezi, na walimu kufahamu Kalenda ya Shule (School Almanac) iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Ratiba hii inahusu shule zote za Msingi na Sekondari nchini Tanzania. Kujua tarehe za kufungua, likizo fupi (Mid-term), na kufunga shule kutakusaidia kupanga mipango yako ya kifamilia na kimasomo mapema bila kuathiri mahudhurio ya mwanafunzi.
Hapa matokeoyanectatz.com, tumekuchambulia ratiba nzima ya mwaka 2026 kwa urahisi.
Muhula wa Kwanza (Term I)
Muhula wa kwanza ndio mwanzo wa mwaka wa masomo. Kwa mwaka 2026, ratiba imepangwa kama ifuatavyo:
-
Kufungua Shule: Shule zinafunguliwa rasmi tarehe 08 Januari 2026 (Kwa wanafunzi wote wanaoendelea) na 13 Januari 2026 (Kwa Kidato cha Kwanza).
-
Likizo ya Muhula (Mid-Term Break): Kutakuwa na mapumziko mafupi kuanzia Machi 2026.
-
Kufunga Shule (Terminal Break): Muhula wa kwanza unatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi Mei au mwanzoni mwa Juni 2026.
-
Likizo ya Mwezi wa Sita: Wanafunzi watakuwa likizo kwa takribani mwezi mmoja kabla ya kuanza muhula wa pili.
Muhula wa Pili (Term II)
Huu ni muhula wa lala salama, hasa kwa madarasa ya mitihani (Darasa la 4, 7, Kidato cha 2 na 4).
-
Kufungua Shule: Masomo yataendelea kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Julai 2026.
-
Likizo ya Muhula (Mid-Term Break): Mapumziko mafupi yanatarajiwa mwezi Septemba 2026.
-
Mitihani ya Taifa:
-
Darasa la Saba (PSLE): Wiki ya pili ya Septemba.
-
Kidato cha Pili & Nne: Kuanzia Oktoba/Novemba.
-
-
Kufunga Shule (Annual Break): Shule zitafungwa rasmi kwa likizo ya mwisho wa mwaka mnamo tarehe 04 au 05 Desemba 2026.
Siku Kuu Muhimu (Public Holidays 2026)
Mbali na likizo za kawaida, shule zitakuwa zimefungwa katika siku kuu zote za kitaifa, zikiwemo:
-
Januari 1: Mwaka Mpya
-
Januari 12: Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar
-
Aprili 7: Karume Day
-
Pasaka & Eid el Fitr: (Tarehe zitategemea mwandamo wa mwezi na kalenda ya kanisa).
-
Aprili 26: Siku ya Muungano
-
Mei 1: Siku ya Wafanyakazi
-
Julai 7: Saba Saba
-
Oktoba 14: Nyerere Day
-
Desemba 9: Siku ya Uhuru
-
Desemba 25 & 26: Krismasi na Boxing Day
Ushauri kwa Wazazi na Wanafunzi
Wizara inasisitiza wazazi kuzingatia tarehe hizi.
-
Mahudhurio: Hakikisha mwanafunzi anaripoti shuleni siku ya kwanza ya kufungua. Kuchelewa kunapunguza muda wa kujifunza.
-
Likizo: Tumia muda wa likizo (haswa Juni na Desemba) kumuongezea mwanafunzi maarifa (Tuition au Masomo ya Ziada) au kukuza vipaji vyake.
Ratiba hii inaweza kubadilika kulingana na maelekezo ya Wizara au dharura.
Ili kuwa wa kwanza kupata mabadiliko yoyote ya ratiba hii, Subscribe kwenye blog yetu au jiunge na kundi letu la WhatsApp hapa chini.
