Form One Joining Instructions 2026

Form One Joining Instructions 2026| Fomu za Kujiunga na Shule (PDF), Fomu za Kujiunga na Kidato cha kwanza 2025/2026

Baada ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutangaza majina ya wanafunzi 937,581 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2026, hatua muhimu inayofuata kwa sasa ni kupata Fomu ya Maelekezo ya Kujiunga na Shule (School Joining Instructions).

Hii ndiyo nyenzo muhimu zaidi kwa mzazi au mlezi kwa sasa. Bila fomu hii, huwezi kujua aina ya sare (uniforms) zinazohitajika, tarehe kamili ya kuripoti kwa shule husika, na mahitaji mengine ya msingi.

Katika ukurasa huu, matokeoyanectatz.com inakupa utaratibu rahisi wa kupakua fomu hizi kwa shule za Bweni na Kutwa nchi nzima.

Joining Instructions Zinapatikana Wapi?

Kwa mwaka huu wa masomo 2026, Serikali imerahisisha upatikanaji wa fomu hizi. Kuna njia kuu mbili za kuzipata:

1. Kupakua Mtandaoni (Tovuti ya TAMISEMI)

Hii ndiyo njia ya haraka zaidi. Fomu za kujiunga (Joining Instructions) zimeambatishwa kwenye mfumo uleule uliotumika kutangaza majina.

Hatua za Kufuata:

  1. Tembelea tovuti ya uchaguzi: selection.tamisemi.go.tz

  2. Chagua Mkoa, Wilaya, na Shule aliyotoka mwanafunzi.

  3. Kwenye orodha ya majina, tafuta jina la mwanao.

  4. Upande wa kulia wa jina la shule aliyopangiwa, kuna maandishi au alama ya kupakua (Download). Bofya hapo kupata fomu ya shule hiyo.

2. Kuchukua Shuleni

Kwa wale ambao hawawezi kupata mtandaoni, fomu hizi pia zinatumwa kwa Wakuu wa Shule za Msingi walikohitimu wanafunzi, pamoja na kupatikana katika ofisi za shule za sekondari walizopangiwa.

Mambo Muhimu Yaliyo Kwenye Joining Instruction 2026

Ukishaipata fomu hiyo, hakikisha unasoma kwa makini vipengele vifuatavyo kabla ya kuanza manunuzi:

  • Tarehe ya Kuripoti: Kumbuka agizo la Waziri ni tarehe 12 Januari (Bweni) na 13 Januari (Kutwa). Hakikisha unazingatia tarehe iliyoandikwa kwenye fomu ili usipoteze nafasi.

  • Sare za Shule (Uniforms): Fomu itaelekeza rangi ya shati, suruali/sketi, aina ya viatu, na nguo za michezo. Zingatia kielelezo (sample) kilichowekwa ili usishone sare zisizokubalika.

  • Michango na Ada: Elimu ni BURE (Hakuna Ada ya Masomo). Hata hivyo, fomu inaweza kuainisha mahitaji binafsi ya mwanafunzi au michango ya hiari iliyopitishwa na bodi ya shule kwa utaratibu maalum.

  • Mahitaji ya Bweni: Kwa wanafunzi wa bweni, angalia orodha ya vitu kama godoro, ndoo, na vifaa vya usafi.

Pakua Joining Instructions Hapa (Kimkoa)

Ili kukurahisishia, hapa chini tumekuorozeshea viungo (links) vya kupata fomu hizi kulingana na Mkoa shule ilipo.

(Bofya Mkoa husika kwenda kwenye mfumo wa kupakua)

Arusha Dar es Salaam Dodoma Geita
Iringa Kagera Katavi Kigoma
Kilimanjaro Lindi Manyara Mara
Mbeya Morogoro Mtwara Mwanza
Njombe Pwani Rukwa Ruvuma
Shinyanga Simiyu Singida Songwe
Tabora Tanga Zanzibar

Unashindwa Kupata Fomu Yako?

Kama unatafuta fomu ya shule maalum na huipati mtandaoni, tafadhali tuandikie jina la shule hiyo na mkoa ilipo kwenye sehemu ya MAONI (COMMENTS) hapa chini.

Timu yetu ya matokeoyanectatz.com itajitahidi kukutafutia na kukuwekea link au maelekezo ya wapi utaipata haraka.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *