Nafasi ya Kazi: Shop Sales Attendant (Wadada)Nafasi ya Kazi: Shop Sales Attendant (Wadada)

Nafasi ya Kazi Shop Sales Attendant (Wadada) – Posta, Dar es Salaam, Ajira mpya Dar es Salaam, Nafasi za kazi mauzo, Ajira za wadada Dar es Salaam, Kazi za madukani Posta, Jobs in Tanzania 2026

Eneo la Kazi: Posta, Dar es Salaam
Kiwango cha Mshahara: TZS 400,000 kwa mwezi
Aina ya Kazi: Muda Kamili (Full Time)

Duka la rejareja (Retail Shop) lililopo maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam, linatafuta Mhudumu wa Mauzo (Shop Sales Attendant) mchapakazi na mbunifu ambaye atasaidia kuendesha shughuli za mauzo na kuhudumia wateja kwa weledi.

(Zingatia: Nafasi hii ni maalum kwa ajili ya WANAWAKE/WADADA pekee ambao wanaishi ndani ya jiji la Dar es Salaam).

Sifa za Mwombaji (Requirements)

Ili kufikiriwa katika nafasi hii, mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Kiwango cha Elimu: Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au zaidi.
  • Ujuzi wa Kidijitali: Awe na uwezo na uelewa wa kuuza bidhaa kupitia mitandao ya kijamii (Social Media Marketing).
  • Tabia na Mienendo: Awe mwaminifu sana, mwajibikaji, na mwenye lugha nzuri ya kuvutia na kujali wateja (Good customer care).
  • Uzoefu: Awe na uzoefu wa kufanya mauzo kwenye maduka. Hiki ni kigezo muhimu sana.
  • Jinsia na Eneo: Awe ni Mwanamke (Mdada) na awe anaishi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Majukumu Yako (Responsibilities)

  • Kupokea, kuhudumia wateja na kufanya mauzo ya moja kwa moja ndani ya duka.
  • Kuweka kumbukumbu sahihi za mauzo ya kila siku na kuandaa ripoti fupi (simple reports).
  • Kusaidia shughuli za uendeshaji wa duka za kila siku ikiwemo usafi na upangaji mzuri wa bidhaa (shop organization).
  • Kubuni na kutumia mbinu mbalimbali za kimasoko ili kuongeza mauzo ya duka.

Jinsi ya Kutuma Maombi (How to Apply)

Maombi yote yatumwe kupitia njia ya WhatsApp pekee. Tafadhali usipige simu, tuma ujumbe mfupi wenye taarifa zako kwenda namba:

📱 WhatsApp: +255 703 854 777

Wakati unatuma ujumbe wako wa kuomba kazi, hakikisha umejumuisha taarifa zifuatazo kwa usahihi:

  1. Majina yako kamili (Full Name)
  2. Umri wako (Age)
  3. Mahali unapoishi kwa sasa (Location)
  4. Kiwango chako cha elimu (Education Level)

Kumbuka: Ni waombaji waliokidhi vigezo pekee ndio watakaowasiliana na kupangiwa usaili.

⚠️ ONYO MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE (FRAUD ALERT):
Matokeoyanectatz.com inapenda kuwatahadharisha waombaji wote wa kazi kuwa MAKINI NA MATAPELI. Hupaswi kutoa kiasi chochote cha pesa, kununua fomu, au kutoa rushwa ya aina yoyote ili kupata kazi. Mchakato wa kuomba kazi ni BURE kabisa. Ukiona mwajiri anakuomba pesa kwa kigezo chochote kile (kama vile ada ya usaili au sare za kazi kabla ya kuajiriwa), ripoti mara moja, huyo ni tapeli!

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *