Nafasi ya Kazi CRDB Bank Tanzania, System AnalystNafasi ya Kazi CRDB Bank Tanzania, System Analyst

Nafasi ya Kazi CRDB Bank Tanzania, System Analyst,Nafasi ya Kazi System Analyst CRDB Bank Tanzania (Aprili 2026)

Je, unatafuta nafasi za kazi Tanzania, hasa katika sekta ya TEHAMA (IT) na kibenki? Benki ya CRDB, kupitia kampuni yake tanzu ya CRDB Insurance, inatangaza fursa mpya ya ajira kwa wataalamu wenye ujuzi na uzoefu kujaza nafasi ya System Analyst (Mchambuzi wa Mifumo). Hii ni fursa ya kipekee kukuza taaluma yako ndani ya moja ya taasisi kubwa za kifedha nchini.

Hapa chini ni maelezo kamili kuhusu nafasi hii, majukumu, sifa zinazohitajika, pamoja na maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi.

Muhtasari wa Kazi

  • Jina la Nafasi: System Analyst

  • Kampuni: CRDB Bank (Kampuni Tanzu: CRDB INSURANCE)

  • Anaripoti Kwa: Meneja wa ICT (Manager ICT)

  • Idadi ya Nafasi: 1

  • Aina ya Ajira: Ya Kudumu (PERMANENT) / Muda Kamili (Full-time)

  • Mwisho wa Kutuma Maombi: 29-04-2026

Lengo Kuu la Kazi (Job Purpose)

Kazi kubwa ya System Analyst ni kuchambua mahitaji ya kibiashara, kusanifu suluhisho za kimifumo, kusaidia mifumo ya kimkakati ya taasisi, na kuhakikisha utekelezaji wake unaendana na malengo ya kampuni.

Mtaalamu huyu atahusika na uboreshaji wa mifumo ya bima, kuunganisha mifumo (API integrations), kufanya majaribio (testing), na kutoa msaada wa kiufundi wa kila siku (application support) kwa mifumo ya kifedha na majukwaa ya kidijitali. Atatumika kama daraja kati ya watumiaji wa mifumo, watoa huduma (vendors), na timu nzima ya ICT.

Majukumu Makuu (Principle Responsibilities)

  • Kukusanya, kuchambua, na kuweka kumbukumbu za mahitaji ya kibiashara kutoka idara za bima (underwriting, claims), fedha, na uongozi.

  • Kuandaa Nyaraka za Mahitaji ya Biashara (BRDs), mtiririko wa kazi (process flows), na maelezo ya kiufundi.

  • Kusaidia upangaji wa miradi na uratibu kati ya timu za ndani na watoa huduma.

  • Kufanya uchambuzi wa mapungufu kwenye mifumo (gap analysis) na kupendekeza suluhisho sahihi.

  • Kutekeleza maboresho madogo kwenye mifumo, ripoti, na kuweka mifumo ijiendeshe yenyewe (automation).

  • Kusaidia marekebisho (customization) kwenye mfumo mkuu wa bima, ERP, na majukwaa ya kidijitali.

  • Kusaidia muunganiko wa mifumo (API integrations) kati ya mifumo mikuu, mifumo ya fedha, simu za mkononi, na washirika wengine (third-parties).

  • Kufuatilia muunganiko huo na kutatua changamoto zozote zinazojitokeza.

  • Kutengeneza na kufanya majaribio ya mifumo (functional, integration, regression, and UAT testing).

  • Kuratibu shughuli za majaribio ya watumiaji wa mwisho (User Acceptance Testing – UAT).

  • Kutoa msaada wa kiufundi ngazi ya pili kwa kutatua changamoto za kiutendaji na kupendekeza suluhisho za kudumu.

Sifa na Vigezo Zinazohitajika (Qualifications)

  • Shahada (Bachelor’s Degree) katika Sayansi ya Kompyuta, IT, Uhandisi wa Programu (Software Engineering), Bima, au fani zinazohusiana.

  • Uzoefu wa angalau miaka 2 hadi 5 katika uchambuzi wa mifumo, na usimamizi wa program za kitaasisi.

  • Uzoefu wa kufanya kazi na mifumo mikuu, ERP platforms, huku uzoefu katika taasisi za kifedha au bima ukipewa kipaumbele zaidi.

  • Uelewa mzuri wa Mzunguko wa Utengenezaji wa Programu za Kompyuta (SDLC).

  • Ujuzi mzuri wa kutumia kanuni za SQL na hifadhidata (database querying), pamoja na uwezo wa kutafsiri mahitaji ya biashara kwenda kwenye maelezo ya kiufundi kama vile REST/SOAP API.

  • Uwezo mkubwa wa kutatua matatizo (problem‑solving), mawasiliano mazuri, na umakini kwenye kazi.

Bonyeza hapa kutuma maombi>> Nafasi ya Kazi System Analyst CRDB Bank Tanzania

Dhamira ya CRDB (CRDB Commitment)

Benki ya CRDB imejidhatiti katika kufuata misingi ya Uendelevu (Sustainability) na mazoea ya ESG. Benki inahamasisha mazingira jumuishi ya kazi; hivyo basi, maombi kutoka kwa wanawake na watu wenye ulemavu yanahimizwa sana.

Zingatia: Benki ya CRDB haitozi ada yoyote katika hatua yoyote ya kutuma maombi au usaili wa kazi. Puzia ombi lolote la pesa kwani haliendi sambamba na taratibu za benki. Waombaji waliokidhi vigezo pekee (Shortlisted Candidates) ndio watakaowasiliana nao.

Jinsi ya Kutuma Maombi na Link ya PDF

Kama unakidhi vigezo vilivyoainishwa hapo juu na uko tayari kuomba nafasi hii ya System Analyst at CRDB Bank, tafadhali fuata maelekezo yafuatayo:

Bofya Hapa Kupakua PDF ya Nafasi ya Kazi System Analyst CRDB Bank Tanzania

Ili kutuma maombi yako moja kwa moja kwenye mfumo wa benki, tafadhali bofya link rasmi hapa chini:  CRDB CAREERS PORTAL

Ili kupata taarifa za ajira mpya Tanzania kila siku, endelea kutembelea website yako pendwa ya matokeoyanectatz.com.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *