Kazi TAKUKURU 2026: Nafasi 250 za Maafisa Uchunguzi II (Investigation Officers)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anawakaribisha Watanzania waliofuzu kuomba nafasi 250 za Maafisa Uchunguzi II (Investigation Officers II). Nafasi hizi ni kwa ajili ya kuimarisha utendaji katika ofisi za wilaya nchi nzima.
Sifa za Kitaaluma (Academic Qualifications)
Waombaji wanapaswa kuwa na Shahada ya Kwanza (Undergraduate Degree) au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambulika katika fani zifuatazo:
-
Uhasibu na Biashara: Accounting, Business Administration, Procurement.
-
Sheria na Jamii: Law, Community Development, Psychology Counselling, Public Administration.
-
Uhandisi na Ujenzi: Civil, Electrical, Mechanical, Water, Building Economics (QS), Architecture.
-
Teknolojia na Takwimu: Computer Science/IT, Statistics, Oil and Gas Engineering.
-
Nyinginezo: Mass Communication, Record Management, Food and Nutrition, Sports Science.
Vigezo vya Ziada:
-
Ufaulu usiopungua Lower Second Class.
-
Ujuzi wa matumizi ya kompyuta (IT).
-
Usajili wa Bodi za Kitaaluma ni sifa ya ziada.
Sifa Nyingine na Masharti (Eligibility)
- Umri: Lazima uwe na umri kati ya miaka 18 na usiozidi miaka 29 ifikapo Mei 2026.
- Uraia: Lazima uwe Raia wa Tanzania.
- Uadilifu: Muombaji awe na uadilifu wa hali ya juu na asiwe na rekodi ya jinai.
- Kituo cha Kazi: Ukiwa miongoni mwa watakaopita, utapangiwa kufanya kazi katika ofisi yoyote ya wilaya ya TAKUKURU.
Nyaraka Muhimu za Kuambatanisha
Unapotuma maombi yako kupitia mfumo wa ajira.pccb.go.tz, hakikisha unaambatanisha nakala zilizothibitishwa (certified copies) za:
-
Vyeti vya Shahada/Advanced Diploma na Transcripts zake.
-
Vyeti vya kidato cha nne (Form IV) na kidato cha sita (Form VI).
-
Cheti cha Darasa la Saba (Standard VII Certificate).
-
Cheti cha Kuzaliwa na Picha moja (Passport size).
-
Namba ya NIDA au Kitambulisho cha Taifa.
-
Barua ya Maombi: Inapaswa kuandikwa kwa mkono (Handwritten) kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
Jinsi ya Kutuma Maombi (Mode of Application)
Maombi yote lazima yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia portal rasmi ya uajiri ya TAKUKURU:
BONYEZA HAPA KUOMBA – ajira.pccb.go.tz
-
Mwisho wa Maombi: Tarehe 03 Mei, 2026.
-
Maelekezo ya Barua: Barua ielekezwe kwa Mkurugenzi Mkuu, TAKUKURU, S.L.P 1291, Dodoma.
Pakua Tangazo la Kazi TAKUKURU (PDF)
Kwa maelezo zaidi ya kitaalamu na fani zote zinazohitajika, pakua nakala rasmi hapa:
DOWNLOAD PDF: INVESTIGATION OFFICERS II POSITIONS – PCCB 2026
Endelea kufuatilia matokeoyanectatz.com kwa ajili ya miongozo zaidi ya ajira, matokeo ya NECTA, na habari za elimu Tanzania.
