Tangazo la Nafasi za Kazi TAKUKURU (PCCB)Tangazo la Nafasi za Kazi TAKUKURU (PCCB)

Tangazo la Nafasi za Kazi TAKUKURU (PCCB) Aprili 2026 – Nafasi 500, Nafasi za Kazi TAKUKURU 2026, Ajira Mpya TAKUKURU Aprili 2026, PCCB Recruitment Portal 2026, Ajira 500 TAKUKURU Tanzania.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU/PCCB) imetangaza kampeni kubwa ya uajiri kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi katika ofisi za wilaya kote nchini Tanzania. Jumla ya nafasi 500 za kazi zimetangazwa kwa ajili ya watanzania wenye sifa za kitaaluma na uadilifu wa hali ya juu.

Mchanganuo wa Nafasi za Kazi Zilizotangazwa

Nafasi hizi zimegawanywa katika makundi makuu mawili kama ifuatavyo:

1. Maafisa Uchunguzi II (Investigation Officers II) – Nafasi 250

  • Sifa za Kitaaluma: Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada (Degree) au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani mbalimbali kama vile Accounting, Law, Engineering, IT, Procurement, Economics, HRM, na nyinginezo.

  • Ufaulu: Angalau daraja la chini la pili (Lower Second Class).

  • Umri: Muombaji awe na umri kati ya miaka 18 na usiozidi miaka 29 ifikapo Mei 2026.

2. Wasaidizi wa Wachunguzi II (Assistant Investigators II) – Nafasi 250

Nafasi hizi ni kwa ajili ya kada mbalimbali za ufundi na utawala, zikiwemo:

  • Ulinzi na Usalama: (Wildlife Management and Law Enforcement/Mgambo).

  • Ufundi wa Magari: (Mechanics/Panel Beating).

  • Udrayva: (Class C).

  • Wasaidizi wa Ofisi na Makatibu Muhtasi.

  • Wahasibu Wasaidizi na Mafundi Kompyuta.

  • Umri: Muombaji awe na umri kati ya miaka 18 na usiozidi miaka 25.

Mahitaji Muhimu na Masharti ya Jumla

Waombaji wote lazima wazingatie masharti yafuatayo:

  • Kuwa na NIDA au namba ya usajili.

  • Barua ya maombi lazima iandikwe kwa mkono (Kiswahili au Kiingereza).

  • Kuambatanisha nakala za vyeti vilivyothibitishwa (Certified Copies) vya elimu na taaluma, ikiwemo cheti cha darasa la saba.

  • Kuwa na uadilifu wa hali ya juu na usiwe na rekodi ya uhalifu.

Jinsi ya Kutuma Maombi (Mode of Application)

Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia mfumo rasmi wa uajiri wa TAKUKURU. Kumbuka, maombi ya barua pepe au ya kupeleka kwa mkono hayatakubaliwa.

  • Tovuti ya Maombi: LINK YA RECRUITMENT PORTAL

  • Barua ya Maombi Ielekezwe kwa:

    Director General, Prevention and Combating of Corruption Bureau (TAKUKURU), P.O. Box 1291, 41101 Dodoma.

Tarehe ya Mwisho (Deadline)

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 03 Mei, 2026. Tunakushauri kuwahi kutuma maombi yako mapema ili kuepuka changamoto za mtandao dakika za mwisho.

Pakua PDF ya Tangazo Kamili la TAKUKURU

Kwa maelezo zaidi kuhusu kila nafasi, sifa mahususi na taratibu za kufuata, tafadhali pakua tangazo rasmi kwa kubonyeza link hapa chini:

DOWNLOAD PDF FILE HERE – TANGAZO LA KAZI TAKUKURU 2026

Endelea kutembelea matokeoyanectatz.com kwa ajili ya updates zaidi za nafasi za kazi, matokeo, na taarifa za elimu nchini Tanzania.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *